Waziri wa Mambo ya Nje wa Abbas Araghchi amefanya ziara katika mji mtakatifu wa Karbala, ambapo alitembelea maqamu takatifu za Imam Hussein ibn Ali na Al-Abbas ibn Ali na kutoa heshima zake wakati wa ziara yake rasmi nchini Iraq.
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran, Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, ameonya kuwa Iran haitakaa kimya mbele ya kuendelea kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon, akilaani mauaji ya raia na ukimya wa baadhi ya mataifa ya Magharibi.