Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Meja Jenerali Ahmad Vahidi, amesema shambulio la kigaidi lililolenga sherehe ya harusi katika eneo la Kohestak nchini Iran limefichua kile alichokiita “uso mwovu na wa kishetani” wa Marekani, akisisitiza kuwa damu ya wahanga wasio na hatia haitapotea bure.
Meja Jenerali Ahmad Vahidi amesema wapiganaji wa Kiislamu, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na kwa kujitolea kwao, waliweza kulazimisha jeshi lenye silaha nyingi zaidi duniani kusalimu amri.