Mwanazuoni wa Kisunni na Imamu wa Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ali Ibn Abi Talib, Molavi Mohammad Anwar Rigi, ameuawa Shahidi baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana katika mji wa Mirjaveh, kusini-mashariki mwa Iran. Mamlaka za eneo hilo zimesema uchunguzi unaendelea kubaini wahusika wa shambulio hilo, huku wananchi wakitakiwa kudumisha utulivu na kutoruhusu tukio hilo kuchochea migawanyiko ya kidini.
Kwa mujibu wa vyanzo vya Kizayuni, katika kuendeleza uvamizi wake ndani ya ardhi ya Lebanon na mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa muqawama, mwanachama wa Kikosi Maalumu cha Ridhwan cha Hezbollah ameuawa shahidi katika shambulizi la anga lililofanywa na Israel katika eneo la al-Qulay‘a, kusini mwa Lebanon.