Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sheikh Mohammad Anwar Riggi, mwanazuoni wa Kisunni na Imamu wa Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ali Ibn Abi Talib, ameuawa shahidi katika shambulio la kigaidi lililotokea katika mji wa Mirjaveh, kusini-mashariki mwa Iran.
Kwa mujibu wa mamlaka za eneo hilo, Sheikh Riggi alilengwa na watu wenye silaha ambao hawajatambulika katika shambulio lililotokea wakati wa usiku. Tukio hilo limetokea katika Mkoa wa Sistan na Baluchestan, eneo linalopakana na Pakistan.
Mamlaka za eneo hilo zimelaani vikali shambulio hilo na kusema kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini waliohusika na tukio hilo. Pia zimewataka wananchi kuwa watulivu na kutoruhusu tukio hilo kutumiwa kuchochea migawanyiko ya kidini au kuvuruga umoja na usalama wa jamii.
Habari hii imeandaliwa kwa kuzingatia taarifa zilizoripotiwa na mamlaka za eneo hilo; hadi sasa hakuna kundi lililotajwa rasmi kuwa limehusika na shambulio hilo.
Maoni yako