Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei
-
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa Iran: Shambulio la Miundombinu Litajibiwa kwa Hatua Kama Hiyo
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohammad Baqer Zolqadr, amesema kuwa shambulio lolote dhidi ya miundombinu ya Iran litajibiwa kwa hatua kama hiyo, akisisitiza kuwa Israel haitakwepa majibu ya wapinzani wake.
-
Mamilioni ya Waumini Washuhudia Mbele ya Mwenyezi Mungu Wema wa Kiongozi Shahidi Kupitia Sala ya Maiti
Mamilioni ya waumini walioshiriki katika mazishi ya Ayatullah Mkuu Sayyid Ali Husseini Khamenei walimwombea dua katika Sala ya Maiti, wakimshuhudia mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa alikuwa mja mwema na kumuombea rehema na daraja ya juu.
-
Mwakilishi wa Ayatollah Sistani Ataongoza Swala ya Janaza ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika Haram ya Imam Hussein (a.s)
Uongozi wa Ataba Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) umetangaza kukamilisha maandalizi yote ya kupokea msafara wa mazishi ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, huku swala ya janaza ikitarajiwa kuongozwa na mwakilishi wa Marjaa Mkuu Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, Sheikh Abdul Mahdi al-Karbala'i.
-
Hawza ya Hazrat Zainab (as) Kigamboni Yaandaa Khatmu ya Qur'an Tukufu kwa Ajili ya Shahidi Sayyid Ali Khamenei na Mashahidi wote wa Vita vya Ramadhan
Wanafunzi wa Hawza ya Hazrat Zainab (as) Kigamboni, wameshiriki katika Khatmu ya Qur'an Tukufu kwa ajili ya kuwaombea Mashahidi wa vita vya Ramadhan, akiwemo Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei.