Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, katika ujumbe wake wa rambirambi kufuatia kuaga dunia kwa Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani, alimuelezea marehemu kuwa miongoni mwa nguzo kuu za ufundishaji wa Fiqhi na Usuli Fiqhi katika Hawza za elimu ya dini.
Sherehe ya kuusindikiza mwili mtukufu wa Ayatullah Al-Udhma Wahid Khorasani itafanyika siku ya Jumatano, tarehe (18 Novemba), katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran.
Ayatullah al-Udhma Sheikh Hossein Wahid Khorasani, miongoni mwa Marjaa wakuu wa Taqliid, amelazwa katika mojawapo ya hospitali za Tehran, na matibabu yake yanaendelea chini ya uangalizi wa madaktari.