4 Novemba 2026 - 12:19
Ayatollah Wahid Khorasani amelazwa hospitalini

Ayatullah al-Udhma Sheikh Hossein Wahid Khorasani, miongoni mwa Marjaa wakuu wa Taqliid, amelazwa katika mojawapo ya hospitali za Tehran, na matibabu yake yanaendelea chini ya uangalizi wa madaktari.

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Habari la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa ofisi ya Ayatullah Wahid Khorasani, Marjaa huyo wa Taqliid amelazwa katika mojawapo ya hospitali za Tehran kwa ajili ya kufanyiwa baadhi ya matibabu, na huduma zake za matibabu zinaendelea chini ya uangalizi wa madaktari.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha