Ayatollah Khamenei amewaombea Marehemu rehma na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na amewatakia familia za wahanga subira na utulivu wa moyo. Vilevile, amewaombea majeruhi wapate uponyaji wa haraka.
Baada ya mlipuko uliotokea jana katika Bandari ya Shahid Rajaei iliyopo katika Mji wa Bandar Abbas, Serikali ya Muda ya Afghanistan, sambamba na mataifa mengi duniani, imetoa pole kwa watu na Serikali ya Iran.