27 Aprili 2025 - 17:03
Serikali ya Muda ya Afghanistan Yatoa Pole kwa Watu wa Iran Kufuatia Mlupuko wa Bandar Abbas

Baada ya mlipuko uliotokea jana katika Bandari ya Shahid Rajaei iliyopo katika Mji wa Bandar Abbas, Serikali ya Muda ya Afghanistan, sambamba na mataifa mengi duniani, imetoa pole kwa watu na Serikali ya Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) — ABNA — Kufuatia mlipuko uliotokea jana (Jumamosi 26 April, 2025) katika Bandari iliyopo katika Mji wa Bandar Abbas, Serikali ya Muda ya Afghanistan imeungana na mataifa mengi ya dunia katika kutoa pole kwa Wananchi na Serikali ya Iran.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Serikali ya Muda ya Afghanistan, kupitia tamko lililotolewa siku ya Jumapili (27 April, 2025), imesema kuwa ina huzuni kubwa juu ya tukio la mlipuko katika Bandari ya Shahid Rajaei, na imetangaza mshikamano wake na familia za waathirika, pamoja na watu na Serikali ya Iran.

Katika tamko hilo, imeelezwa kuwa katika kipindi hiki kigumu, watu wa Afghanistan na Serikali ya muda wamesimama bega kwa bega na watu na Serikali ya Iran, na wametangaza mshikamano na msaada wao kamili kwao.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha