Mahakama ya Jinai ya Nne mjini Damascus imeanza kusikiliza kesi dhidi ya aliyekuwa Mufti wa Jamhuri ya Syria, Ahmad Hassoun, anayekabiliwa na tuhuma za kuchochea mauaji, kuhalalisha uhalifu wa kivita na kutoa uungwaji mkono wa kidini na kisiasa kwa utawala wa zamani wa Bashar al-Asad na washirika wake.
Baada ya kuanguka kwa serikali ya Bashar al-Assad mwezi Desemba 2024, jamii ya Waalawi wa Syria ilikumbwa na wimbi la vitisho vya kiusalama, kiuchumi na kisiasa.
Kama jibu kwa hali hiyo, viongozi wa kidini na kisiasa wa kundi hili walianzisha baraza mbalimbali kwa lengo la kutetea haki za Waalawi na kufasili upya nafasi yao ndani ya muundo wa kisiasa wa Syria ya baadaye.