Beiruti
-
Dkt. Hossam Matar: “Rais wa Jamhuriya si Dola, na tunakataa kujisalimisha”
Dkt. Hossam Matar amemkosoa Rais wa Lebanon kuhusu namna anavyotekeleza madaraka yake, akisisitiza kuwa rais ni sehemu ya mamlaka ya nchi anayefungwa na Katiba. Amesema suluhu ya kisiasa inapaswa kulinda mamlaka na haki za Lebanon, badala ya kuwa “kujisalimu” mbele ya shinikizo la Marekani.
-
Uchambuzi: Mashambulizi ya Beirut na Mvutano Mpya wa Kikanda
Kinachoendelea katika shambulizi la Israel dhidi ya Beirut ni kama ifuatavyo: Mashambulizi ya Israel Kusini mwa Beirut yanaonyesha kuendelea kwa mivutano ya kikanda, huku ukiwepo msisitizo kuwa Muqawama - Upinzani- wa Lebanon (Hezbollah) unaona una uhalali wa kukabiliana na jaribio lolote la adui Israel katika kubadilisha mlingano wa usalama katika nchi ya Lebanon.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Akutana na Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kishia Lebanon Beirut
Wakati wa ziara yake rasmi mjini Beirut, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Seyyed Abbas Araghchi, alikutana na Sheikh Ali Al-Khatib, Naibu Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia nchini Lebanon. Mazungumzo yao yalijikita katika maendeleo ya kikanda, umuhimu wa umoja wa Kiislamu, na kuimarisha ushirikiano wa kidini na kisiasa kwa ajili ya uthabiti na mshikamano wa Lebanon.