Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya kimataifa na kisheria, Kazem Gharibabadi, amesema hadhi na usimamizi wa Mlango wa Hormuz hauamuliwi na Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM), akisisitiza kuwa usalama wa eneo hilo unategemea kuheshimiwa kwa mamlaka ya mataifa ya kanda.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baghaei, amesema mkutano wa kile kilichoitwa "Mazungumzo ya Usalama wa Kikanda" ulioandaliwa na Marekani nchini Bahrain ni wa maonyesho tu na unalenga kuficha sera ambazo, kwa mujibu wake, zinachochea ukosefu wa utulivu katika eneo la Asia Magharibi.