Makundi ya Muqawama nchini Iraq yametoa onyo kali kwa serikali ya mpito ya Syria, yakisema kuwa ushirikiano wowote wa kijeshi au kiusalama na Marekani na Israel dhidi ya Hizbullah ya Lebanon utakabiliwa na jibu la kijeshi.
Uchunguzi mpya wa maoni nchini Lebanon umeonyesha kuwa Wana-Lebanon wengi—bila kujali dini au dhehebu—wanapinga kuondolewa silaha za vikosi vya mapambano bila kuwepo mkakati mbadala wa ulinzi.