Mwalimu wa Chuo cha Dini cha Qom amesema kwamba akili bandia (AI) imeunda mipaka mipya katika eneo la uwajibikaji, mamlaka, na haki. Aliongeza kuwa: Fiqh inapaswa kuwa na mtazamo wa kuangalia mbele, ili iweze kutoa hukumu na msingi wa dini kwa matukio mapya kabla ya kuibuka kwa migogoro au majanga.
"Kazi kuu na ya msingi ya Hawza ni (البَلاغُ المُبین) kufikisha ujumbe wa dini kwa uwazi na ufasaha (ubalighi wa wazi - Kwa maana: Kufikisha ujumbe kwa uwazi na uthabiti na kwa namna ambayo haiachi shaka yoyote -). Miongoni mwa vielelezo vyake muhimu kabisa ni kuchora na kueleza kwa uwazi mistari (mipaka) mikuu na ya kando ( au midogo) ya ustaarabu mpya wa Kiislamu, pamoja na kuifafanua, kuieneza, na kuikuza katika jamii kama sehemu ya utamaduni."