Saudi Arabia imefanya kosa la kimkakati katika kutathmini maslahi ya uhusiano wake na Trump. Riyadh ilidhani kuwa ingeweza kutumia mahusiano ya kifedha na binafsi kuelekeza sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa manufaa yake, bila kubeba gharama zinazotokana na ufisadi, ukosefu wa utulivu na maamuzi hatarishi ya Washington. Hata hivyo, kwa sasa, kutokana na kuongezeka kwa vitisho vya kiusalama na shinikizo dhidi ya miundombinu yake ya kiuchumi, Saudi Arabia inakabiliana na matokeo ya hesabu hiyo ya kimkakati iliyokosewa.
Jarida la Foreign Policy limeeleza kuwa vita dhidi ya Iran vimekuwa “janga la kimkakati” kwa Washington, likisema Marekani imeshindwa kufikia malengo yake makuu ya kimkakati. Jarida hilo pia limekosoa madai ya Donald Trump kuhusu “ushindi” na kueleza kuwa mapigano yanaendelea huku kukiwa hakuna dalili wazi ya makubaliano kati ya Washington na Tehran.