Duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya chama cha Likud kinachoongozwa na Benjamin Netanyahu na chama cha Yashar kinachoongozwa na Gadi Eisenkot, kuhusu kuunda serikali ya umoja, ilimalizika bila kufikiwa kwa makubaliano. Hali hii imekuja huku tofauti kuhusu nani atakayekuwa Waziri Mkuu ajaye na muundo wa Baraza la Mawaziri la utawala wa Kizayuni (Israel) zikiendelea kuwepo.
Gadi Eisenkot, kiongozi wa chama cha Yashar na mteuliwa wa kuunda baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel, akijibu hotuba ya Benjamin Netanyahu bungeni (Knesset), amesisitiza kuwa amezidi kushawishika kwamba Netanyahu hastahili kuendelea kushikilia wadhifa wake hata kwa dakika moja zaidi. Aidha, amezitaka vyama vinavyounda muungano wa serikali kuchukua hatua mara moja za kuunda serikali ya dharura.