Guantanamo
-
Wafungwa watano wahamishwa kutoka Guantanamo
Wizara ya ulinzi ya Marekani Pentagon, imesema kwamba wafungwa watano katika gereza la Marekani la Guantanamo wamepelekwa katika nchi nyengine. Wanne kati ya hao wamepelekwa Oman na mwengine nchini Estonia.
-
Serikali ya Marekani yawaachia huru wafungwa 64 wa Guantanamo
Serikali ya Marekani imesema kwamba wafungwa 64 kati ya 132 wanaobakia katika gereza ka Guantanamo Bay wanaweza kuondoka katika gereza hilo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya nchi hiyo Marie Harf amesema Marekani inasubiri nchi nyingine zikubali kuwapokea wafungwa hao.
-
Bunge la Uingereza kuchunguza ripoti ya mateso ya gereza la Guantanamo
Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ilio na nguvu nchini Uingereza amesema, kamati hiyo inaiomba Marekani kuwasilisha sehemu iliofichwa ya ripoti ya mateso yaliodaiwa kufanywa na maafisa wa Marekani wa shirika la ujasusi CIA
-
Shirika la kijasusi la Marekani lajitetea kuhusu mateso ya Guantanamo
Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), John Brennan, amelitetea shirika lake dhidi ya tuhuma za Baraza la Seneti kwamba wamekuwa wakitumia mateso ya kikatili kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi.
-
Radi amali za viongozi mbali mbali kuhusu mateso ya gereza la Guantanamo
Mateso yanayofanywa na serikali ya marekani dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi walioko katika gereza la Guantanamo imeonekana kuwa ni unyama wa hali ya juu na ukiukaji wa haki za binadamu, viongozi wengi duniani wamesikitishwa sana na ukatili huo unaofanya na serikali ya Marekani.
-
Ripoti kuhusu udhalilishaji na mateso wanayopata wafungwa wa Guantanamo
Kamati ya seneti ya Marekani inayoshughulikia masuala ya upelelezi inatarajia kuchapisha ripoti juu ya mbinu zilizotumiwa na shirika la ujasusi CIA katika kuwahoji watuhumiwa wa ugaidi kwenye jela ya Guantanamo.
-
Watuhumiwa wa ugaidi sita wa Guantanamo waachiwa huru
Marekani imewaachia huru wanafungwa sita ambao walikuwa ni watuhumiwa wa ugaidi na kuwapeleka katika nchi ya Uruguay kama wakimbizi huru, hii inahesabika kuwa ni hatua ya rais wa Marekani katika kuonyesha dhamira ya kulifunga gereza hilo la kutisha.