Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ilio na nguvu nchini Uingereza amesema, kamati hiyo inaiomba Marekani kuwasilisha sehemu iliofichwa ya ripoti ya mateso yaliodaiwa kufanywa na maafisa wa Marekani wa shirika la ujasusi CIA, ili kujaribu kugundua iwapo maafisa wa ujasusi wa Uingereza walichangia katika mateso hayo au mpango wake wa kuwarudisha watuhumiwa katika nchi wanakotafutwa. Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya ujasusi na usalama Sir Malcolm Rifkind amesema iwapo kamati hiyo itapata ushahidi wa kuhusika kwa maafisa wake, inaweza kuwahoji wanasiasa kutoka chama cha labour kama vile Waziri Mkuu wa zamani Tony Blair waliokuwa madarakani wakati wa madai ya mateso hayo. Wiki iliopita, ripoti iliotolewa na baraza la seneti la Marekani, iligundua maafisa wa CIA wa Marekani waliipotosha Ikulu ya nchi hiyo pamoja na umma juu ya mateso ya washukiwa wa ugaidi baada ya shambulio la Septemba 11 mwaka wa 2011 na kwamba mateso hayo yalikuwa ya ukatili mkubwa kuliko ilivyofikiriwa.
Mateso yaliyosikika kutokea katika gereza la Guantanamo ni sehemu ndogo tu ya mateso hayo ya kinyama yaliyofanywa na serikali ya Marekani dhidi ya haki ya binadamu, ukali wa ripiti hiyo umepelekea serikali ya Marekani kuficha ukali wa ripoti hiyo na kutoa sehemu ya ripoti isiyokuwa na madhara kwa taifa hilo, Uingereza imeingiwa na wasiwasi kwani nayo ilishiriki katika mateso hayo ya kinyama, ambayo yanahofiwa kuleta kisasi na chuki dhidi ya serikali na raia wa Marekani.