Baadhi ya viongozi wa kisiasa wa Uingereza, wakiwemo Waziri Mkuu wa nchi hiyo, wametuma salamu za pongezi kwa Waislamu wa Uingereza na ulimwenguni kote kwa mnasaba wa Sikukuu ya Eid al-Adha.
Serikali ya Uingereza imeamua kusitisha mazungumzo ya mkataba wa biashara huria na utawala wa Kizayuni kutokana na kuongezeka kwa ghasia zinazofanywa na wakazi wa maeneo ya mizozo na uendeshaji wa operesheni za kijeshi katika ukanda wa Ghaza. Aidha, imeweka vikwazo dhidi ya watu na mashirika yanayohusiana na ghasia hizi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza pia amemwita balozi wa utawala huo ili kutoa maelezo kuhusu hali hiyo na kusisitiza umuhimu wa kuacha mara moja matendo ya ukatili.