16 Machi 2025 - 15:53
Onyo la Baraza la Wawakilishi la Yemen: Vikosi vya jeshi vitajibu ipasavyo

Baraza la Wawakilishi la Yemen limetoa taarifa likionya kuhusu matokeo ya hujuma za Marekani na Uingereza dhidi ya raia wa nchi hii.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul -Bayt (AS) - Abna - Baraza la Wawakilishi la Yemen limetoa taarifa kujibu hujuma ya jana usiku ya Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo ya makazi ya nchi hii na kuonya juu ya matokeo ya kuendelea kwa hujuma hizo.

Imesisitizwa katika taarifa hiyo kuwa: Kuwalenga raia ni uhalifu kamili wa kivita; ni Jinai ambayo inafanywa na utawala huo kwa ajili ya kumuunga mkono adui Mzayuni na kuwaua Wapalestina na wananchi wa eneo hili (la kikanda) hususan katika nchi za Lebanon na Syria.

Katika muendelezo wa kauli hiyo imeelezwa kuwa: Jinai hizo ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya Yemen na Sheria za Kimataifa, na vikosi vya jeshi vya nchi hii vina haki ya kuonyesha jibu linalofaa dhidi ya vitendo vya kigaidi vya Marekani na Uingereza.

Baraza la Wawakilishi la Yemen limeitaka Jumuiya ya Kimataifa kutekeleza majukumu yake ya kibinadamu na kimaadili dhidi ya jinai hizo. Mabunge ya nchi za Kiarabu na Kiislamu pia yanapaswa kulaani hujuma hizi.

Mashambulizi ya ndege za kivita za wavamizi dhidi ya maeneo ya makazi ya raia wa Yemen yamesababisha zaidi ya Mashahidi 130 na wengine wengi kujeruhiwa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha