Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Leo hii (jana: 17/3/2025) kumefanyika tukio muhimu kwa wafuasi wa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s) Jijini Arusha, nalo ni ufunguzi wa Husseiniyyah Mpya kwa jina la Imamu Ridha (a.s), chini ya Usimamizi wa Taasisi ya Sayyid al-Shuhadaa (a.s), inayoongozwa na Samahat Sheikh Maulid Hussein Kundya.
Wasomaji wa Kitaifa na Kimataifa wa Qur'an Tukufu wa Tanzania pamoja na Masheikh waliotoka maeneo mbalimbali ya nchi, ni miongoni mwa waliodhuhuria katika Hafla hiyo adhimu ya Ufunguzi wa Husseiniyyah ya Aba Abdillah Al-Husseini (a.s) iliyopewa jina la Imam Ridha (a.s), ambaye ni Imam wa nane kati ya Maimam Kumi na Wawili (a.s) wa Kizazi Kitukufu cha Mtume wetu Muhammad (s.a.a.w).
Your Comment