18 Machi 2025 - 00:23
Ni kwa nini Mashia tu ndio wako mstari wa mbele kwenye kulitetea suala la Palestina?!

Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge: "Uislamu usiokuwa wa Ahlulbayt wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), huo umetengenezwa na Mayahudi au kama haukutengenezwa na Mayahudi basi umeingizwa mikono kwa asilimia 99% na Mayahudi".

Kwa Mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA -: Maulana Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C), katika Darsa lake la Tafsiri ya Qur'an Tukufu amejibu swali aliloulizwa na baadhi ya Waumini wa Kiislamu kwamba: Ni kwa nini ni Mashia tu ndio wako Mstari wa mbele kwenye kulitetea jambo la Palestina?!.

Samahat Sheikh Hemed Jalala akijibu swali hilo amesema: "Mashia wako Mstari wa mbele kuitetea kadhia ya Palestina kwa sababu Mashia ndio Uislamu pekee na Madhehebu pekee ambayo haikutengenezwa na Mayahudi. Na maneno haya yanaweza kuonekana ni maneno mazito, lakini hatuna ni lazima tuyaseme ili kufahamisha.

Uislamu usiokuwa wa Ahlulbayt wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), huo umetengenezwa na Mayahudi au kama haukutengenezwa na Mayahudi basi umeingizwa mikono kwa asilimia 99% na Mayahudi.

Ni kwa nini Mashia tu ndio wako mstari wa mbele kwenye kulitetea suala la Palestina?!

Ikutoshe kama ushahidi kwako wewe muuliza swali na nyinyi nyote mlioko hapa: Tizameni leo hii Duniani nani anajali (kadhia) suala la Palestina?!. Hata Mwenye Misikiti yetu suala la Palestina haliguswi wala kusemwa!.

Mwisho, Maulana Sheikh Hemed Jalala Mwakindenge amegusia suala la Syria na kusema: Wale wanaoitwa leo hii kuwa Wanajihadi (Mujahidina) huko Syria, walioenda na kuipindua Serikali halali ya Rais Bashar Al_Asad, hapo awali walikuwa wakiizungumzia Palestina, lakini jiulize je, leo hii wanaizungumzia tena Palestina?!. Wanao tena mpango wowote ule kuihusu Palestina?! Wana lolote lile kuhusu Masjid Al-Aqsa?!.

Ni kwa nini Mashia tu ndio wako mstari wa mbele kwenye kulitetea suala la Palestina?!

Leo hii, Palestina Masunni wanapigwa ndani ya Msikiti wasiswali Tarawehe, sio Imam wa Makkah au Madina, au yeyote anayewatetea Masunni wa Palestina wasiswali Swala ya Tarawehe Msikitini!.Hakuna!.

Ni kwa nini Mashia tu ndio wako mstari wa mbele kwenye kulitetea suala la Palestina?!

Usunni au Ahlu_Sunna, hawawezi kamwe kuwatetea Masunni wa Palestina, au hata kuwasema Mayahudi, kwa nini?! Ni kwa sababu Mfumo wa Usunni ulivyotengenezwa, ndani yake kuna mikono ya Mayahudi".

Mwisho wa kunukuu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha