Admirali Habibollah Sayyari amesema vikosi vya ulinzi vya Iran viko katika utayari kamili wa kulinda mipaka na mamlaka ya nchi, akisisitiza kuwa jaribio lolote la kuivamia Iran litashindwa na kujibiwa kwa nguvu.
Msaidizi wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran, Admirali Habibollah Sayyari, amesema kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vina vifaa vya kisasa na vipo tayari kukabiliana na tishio lolote, huku akisisitiza kwamba adui yeyote atakayeshambulia Iran atakabiliwa na jibu kali zaidi kuliko hapo awali.