Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq imemuita balozi wa Uingereza mjini Baghdad kutokana na matamshi yake kuhusu nafasi ya Hashd al-Shaabi katika mfumo wa usalama wa Iraq, na imeonyesha majibu makali juu ya kauli hizo.
Kiongozi wa Harakati ya Hekima ya Kitaifa ya Iraq amesisitiza umuhimu wa Hashd al-Shaabi katika kulinda nchi ya Iraq na ametoa wito wa kuendelezwa kwa juhudi za kiusalama pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa katika uwanja huo. Sayyid Ammar Hakim pia ameashiria kujitolea kwa Hashd al-Shaabi na nafasi yake katika kuleta uthabiti nchini Iraq, na amesisitiza ulazima wa kulinda heshima na sifa njema ya taasisi hiyo.