Kikao cha Kursi Tilawat Fatimiyya kinafanyika katika ukumbi wa Imam Khomeini (RA), ndani ya Haram Tukufu ya Hazrat Fatima Masuma (SA), kikihusisha usomaji wa Qur’ani Tukufu kutoka kwa msomaji wa kimataifa wa Qur’ani, Sayyid Muhammad Madani, ufafanuzi wa aya za Qur’ani kutoka kwa Hujjatul-Islam wal-Muslimin Ali Khalilpour, usomaji wa Qur’ani kutoka kwa kijana Mahdi Ebrahimi, pamoja na maonesho ya kikundi cha uimbaji.
Wanafunzi wa Jamiat Al-Mustafa Dar es Salaam wamehuisha mnasaba wa kifo cha Hazrat Fatima Maasuma (sa), binti wa Imam Mussa Al-Kadhim (as), kupitia khutba iliyotolewa na Sheikh Taqee Zakaria, iliyojikita katika maisha yake, safari yake kutoka Madina kuelekea Iran, nafasi yake ya kielimu na kidini, lakabu ya “Maasuma”, fadhila za kumzuru pamoja na nafasi yake katika shafaa Siku ya Kiyama.