Hukumu za Kiislamu zinakutaka Muislamu Itikadi yako iwe ni Itikadi sahihi. Na Uislamu unatufndisha kuwa haijuzu kwa Muislamu yeyote kumfuata (Kumqalid) mtu kuhusiana na suala la Kiitikadi, kwa maana kwamba: Lolote linalohusiana na itikadi, inabidi Muislamu ulikubali na kuliitikadia kwa kutegemea dalili na uthibitisho madhubuti ima wa: Qur’an Tukufu, au Hadithi na Sunna za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake na Aali zake) na Riwaya mbalimbali za Maimam watoharifu (amani iwe juu yao), au uwe ni uthibitisho unaotokana na dalili za kiakili.