Amesema kuwa uongo mwingi kuhusu Iran unatolewa na taasisi zinazopingwa na msimamo wa Iran wa kusimama dhidi ya Marekani na Israel. Hata hivyo, baada ya vita vya siku kumi na mbili, wanafikra wengi duniani wamekiri wazi kwamba Iran ndilo taifa pekee lililosimama dhidi ya dhulma kwa njia ya kivitendo, si kwa maneno tu.
"Ni kweli kwamba usitishaji wa vita umewapa Wapalestina muda wa kupumua, lakini tunapaswa kuwa waangalifu dhidi ya mpango wa kibepari wa Trump. Haiwezekani Marekani - ambayo ni mshirika mkuu katika mauaji ya Wapalestina - kuwa msuluhishi wa haki. Katika mpango wa vipengele 20 wa Trump, hakuna popote palipotajwa uhuru wa Palestina.”