Iran imeishutumu Marekani na Israel kwa kile inachokiita mauaji ya watoto wasio na hatia kupitia vita, mashambulizi na ukaliaji katika maeneo mbalimbali, ikisisitiza kuwa watoto ndio wahanga wakuu wa migogoro inayoendelea duniani.
Ismail Baqaei amesema taarifa ya Umoja wa Ulaya ya kulaani hatua za Iran za kujibu mashambulizi ya Marekani inaonyesha unafiki na viwango viwili, akisisitiza kuwa Iran ilitumia haki yake halali ya kujilinda kwa mujibu wa sheria za kimataifa.