Utekelezaji wa kanuni mpya za mavazi katika shule za umma za Jamhuri ya Azerbaijan umegeuza masuala matatu ya hijabu, haki ya kupata elimu na mfumo wa utawala usioegemea dini kuwa mgogoro wa kisera; mgogoro ambao madhara yake yanaathiri kwa kiasi kikubwa mustakabali wa wanafunzi wa kike wanaovaa hijabu.
Mzunguko mpya wa serikali ya Jamhuri ya Azerbaijan wa kupambana na maadili yanayokubaliwa na Waislamu wengi wa Kishia nchini humo umegeuka siku hizi kuwa habari kuu ya kijamii katika eneo hilo na ulimwengu wa Kiislamu. Hata hivyo, hadi sasa, mwitikio mkubwa zaidi kutoka nje ya nchi umetolewa na Uturuki, mshirika wa karibu, rafiki na mshirika wa kimkakati wa Jamhuri ya Azerbaijan.
Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kupitia Tamko la Baku limesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarisha sekta za ubunifu na diplomasia ya kitamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu.