Chama cha Al-Wefaq, kimelaani hukumu zilizotolewa dhidi ya Sheikh Isa Qassim pamoja na kundi la wanazuoni na viongozi wa kidini nchini Bahrain, kikieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuongezeka kwa mashinikizo ya utawala dhidi ya wapinzani wa sera za utawala wa Kizayuni (Israel).
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Al-Wefaq nchini Bahrain amefichua madai ya kuhamishwa kwa taarifa na data za raia wa Bahrain kwenda kwa utawala wa Israel. Ameeleza kuwa suala hilo linahusiana na mabadiliko ya kiusalama katika eneo hilo na vita dhidi ya Iran. Aidha, amekosoa hatua za kiusalama za Manama na shinikizo linalodaiwa kuelekezwa dhidi ya jamii ya Kishia nchini Bahrain, huku akionya kuhusu athari za ushirikiano wa kiusalama na utawala wa Israel kwa usalama wa raia wa Bahrain.