Wizara ya Usalama ya Iran imetangaza kukamatwa kwa watu wanne wanaodaiwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi na kuuawa kwa wengine wawili wakati wa mapambano na vikosi vya usalama katika mji wa Khash, mkoani Sistan na Baluchestan.
Shirika la Habari la Mehr limechapisha maelezo ya rasimu ya makubaliano yenye vipengele 14 kati ya Iran na Marekani, ikijumuisha kusitishwa kwa vita, kuondolewa kwa vikwazo, kufunguliwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, kurejeshwa kwa fedha za Iran na mazungumzo kuhusu nyuklia, huku ikisisitiza kuwa mpango wa makombora wa Iran na uhusiano wake na Muqawama havitakuwa sehemu ya makubaliano hayo.