Katika maadhimisho ya miaka mitatu ya Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa, matokeo ya utafiti wa maoni uliofanywa na Kituo cha Pew yanaonyesha kuwa baadhi ya mabadiliko yaliyotokea yanaendana na malengo ya Yahya Sinwar. Mtazamo hasi wa watu duniani kuhusu utawala wa Israel umefikia asilimia 67, huku nafasi ya Benjamin Netanyahu katika maoni ya umma duniani ikiwa imeathirika kwa kiasi kikubwa.
Kiongozi wa Harakati ya Hamas, katika Ukanda wa Ghaza, katika Kongresi ya 34 ya Taifa ya Kiarabu huko Beirut, alieleza kuwa Operesheni “Tofaan Al-Aqsa / Kimbunga cha Al-Aqsa” ilikuwa jibu kwa juhudi za kuondoa suala la Palestina na kubuni Mashariki ya Kati mpya, na alisisitiza uhitaji wa kuimarisha uwezo wa upinzani.