Gadi Eisenkot, kiongozi wa chama cha Yashar na mteuliwa wa kuunda baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel, akijibu hotuba ya Benjamin Netanyahu bungeni (Knesset), amesisitiza kuwa amezidi kushawishika kwamba Netanyahu hastahili kuendelea kushikilia wadhifa wake hata kwa dakika moja zaidi. Aidha, amezitaka vyama vinavyounda muungano wa serikali kuchukua hatua mara moja za kuunda serikali ya dharura.
Kura za maoni kuhusu uchaguzi katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu zinaonyesha kuwa muungano pinzani wa Benjamin Netanyahu unaweza kupata viti 56, dhidi ya viti 50 vya chama cha Likud. Hata hivyo, kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa, hakuna upande wowote kati ya miungano hiyo miwili unaofikia idadi ya chini ya viti 61 vinavyohitajika kuunda serikali.