Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema udhaifu wa kijasusi wa Marekani na tathmini zake potofu umeisababisha kufanya makosa makubwa, akisema vita dhidi ya Iran ni mfano wa wazi wa makosa hayo.
Kamanda wa Vikosi vya Ardhi vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Mohammad Karami, amesema vikosi vyao vinaendelea kuwa katika kiwango cha juu cha utayari wa kiintelijensia na kiutendaji ili kukabiliana na tishio lolote kutoka kwa maadui wa nje au makundi ya kigaidi.