Katibu Mkuu wa Hezbollah, Sheikh Naim Qassem, ameonya kwamba kundi la mapambano lina haki ya kulipiza kisasi kutokana na kuuawa kwa kamanda mwandamizi Haitham Al-Tabtabai, na akasisitiza kuwa kujisalimisha si chaguo kabisa.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alisema: Gharama ya kujisalimisha ni kupoteza utambulisho wa kitaifa, utambulisho wa kidini, utambulisho wa kibinafsi, na hata utu wa kibinadamu. Mwanadamu, hata akilipa gharama ya kusimama imara (kupinga), ni bora kuliko kulipa gharama ya kujisalimisha.