Iran imelaani vikali madai ya Waziri Mkuu wa Israel kuhusu umiliki wa kudumu wa Milima ya Golan na kukataa kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina, ikisisitiza kuwa hatua za kikoloni haziwezi kubadilisha ukweli wa kihistoria na kisheria.
Jenerali Amir Hatami amesema adui sasa ametambua kuwa hana budi kuheshimu Taifa la Iran na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, akisisitiza kuwa msimamo na uthabiti wa wananchi wa Iran umebadili hesabu za wapinzani wao.