Msemaji wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (s) amesema madai ya Marekani kuhusu usafiri wa kawaida wa meli kupitia Mlango wa Hormuz ni ya uongo, akisisitiza kuwa Iran inadhibiti na kusimamia kikamilifu eneo hilo.
Mwanaharakati wa vyombo vya habari kutoka Urusi amesema umati mkubwa wa wananchi waliojitokeza kumuaga kiongozi wao umeandika historia, akisisitiza kuwa mshikamano wa Wairani umeonyesha mapenzi ya dhati kwa taifa na uongozi wao.