Dk. Ali Matar, mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na mtafiti wa masuala ya uhusiano wa kimataifa na sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Lebanon, amesisitiza kuwa kukiri kwa Donald Trump kuhusu ushiriki wa Marekani katika vita dhidi ya Iran ni ushahidi rasmi wa uvamizi na uvunjaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Vyombo vya habari vya Israel vimetangaza leo kwamba kutokana na hati ya kukamatwa iliyotolewa dhidi ya Waziri Mkuu wa utawala huu, ndege iliyombeba ilibidi ichukue njia ndefu zaidi kuelekea Washington.