Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Wakati Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliposafiri hadi Washington siku ya Jumatatu kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump, gazeti la Kiebrania Haaretz liliandika kuhusiana na hilo leo hii kwamba: Ndege ya Netanyahu ililazimika kusafiri kwa umbali mrefu kutokana na hati ya kukamatwa iliyotolewa dhidi yake.
Kuhusiana na hilo, Haaretz liliandika: Ndege iliyombeba Netanyahu imesafiri karibia kilomita 400 katika safari yake kutoka Budapest, Mji Mkuu wa Hungary hadi Washington, ili kuepuka (kukwepa) kuruka juu ya anga ya nchi zilizokuwa zikipanga kutekeleza hati ya kukamatwa kwa Netanyahu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
Netanyahu amepanga kukutana na Trump leo Mjini Washington, mada ya mkutano huu haijatangazwa, lakini Netanyahu aliwahi kuzungumzia ushuru wa forodha wa Marekani, Iran na kurejea kwa wafungwa wa Kizayuni kutoka Gaza.
Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni alitangaza madhumuni ya safari hii na kukutana na Trump ili kuchunguza suala la kuwarejesha wafungwa wa Kizayuni kutoka Ghaza na kukamilisha kile alichokitaja kuwa ni "ushindi".
Gazeti la Kiebrania "Yediot Aharonot" liliandika: Trump atakutana na Netanyahu saa kumi na mbili jioni kwa saa za GMT (Greenwich Mean Time).
Gazeti hili la Kiebrania lilizidi kunukuu baadhi ya vyanzo na kuandika kuwa: "Steve Witkoff", Mjumbe wa Marekani katika Mashariki ya Kati, pia atakuwepo katika mkutano wao.
Vyanzo vya Habari vilitangaza kwamba Netanyahu aliwasili Marekani mapema kuliko ilivyopangwa.
Katika mkesha wa safari yake mjini Washington, Netanyahu aliwaambia waandishi wa habari: "Kwa mwaliko wa Rais Trump, ninaenda Marekani kuzungumzia suala la wafungwa, kukamilika kwa ushindi wa Gaza, na pia ushuru ambao Israel imetozwa." Natumai naweza kusaidia katika uwanja huu."
Your Comment