Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, amesema Tehran iliziarifu rasmi nchi jirani kuwa silaha zozote za Marekani zitakazoingia Iran kupitia Ardhi zao, Ardhi hizo zitachukuliwa kuwa sehemu ya uwanja halali wa kujilinda wa Iran.
Vikwazo vilikusudiwa kuinyima Iran ushirikiano wa kimataifa, lakini matokeo yakawa tofauti. Wakati Washington ilipokuwa ikijaribu kuikata Iran na dunia, shinikizo hilo hilo liliisukuma Tehran kufungua njia mpya za ushirikiano na Mashariki, majirani zake, na nchi za Kusini mwa Dunia (Global South). Leo, Iran iko si tu katika moyo wa mtandao wa nishati wa Mashariki ya Kati, bali pia ni mchezaji muhimu katika siasa za Asia, Caucasus, na Ghuba ya Uajemi.