Mapato

  • Jitahidi; Lakini Usiwe na Pupa Juu ya Riziki

    Jitahidi; Lakini Usiwe na Pupa Juu ya Riziki

    “Jua kwamba riziki iko katika aina mbili: Aina ya kwanza ni riziki ambayo unatakiwa kuitafuta na kuifuata [na ni lazima uitafute]; na aina ya pili ni ile riziki ambayo itakujia yenyewe. Hata kama hutaifuata, yenyewe itakufuata.” Inapaswa kufahamika kwamba katika kutafuta riziki, mwanadamu hapaswi kuwa na pupa, wala kuwa mzembe na mvivu. Kwa hiyo, anapaswa kujituma katika kazi na shughuli zake za kila siku. Hata hivyo, kuna aina ya riziki kama vile urithi, ambayo humfikia mwanadamu bila yeye kufanya juhudi yoyote ya kuipata. Kwa hivyo, mwanadamu hapaswi kukata tamaa anapopungukiwa na riziki ya aina ya kwanza, bali anapaswa kuendelea kujitahidi na kufanya kazi, huku akitarajia pia riziki ambazo humjia bila yeye kuzitafuta au kuzipangia.