Marais wa Benki Kuu za Iran na Urusi wamehimiza kuimarishwa kwa ushirikiano wa kifedha, kupanuliwa kwa biashara baina ya nchi hizo mbili, na kuendelezwa kwa Mradi wa Ukanda wa Kaskazini (North Corridor) ili kurahisisha miamala ya kiuchumi.
Utafiti wa pamoja wa The Economist na YouGov umeonyesha kuwa umaarufu wa Donald Trump umeendelea kushuka, huku vita dhidi ya Iran na changamoto za uchumi zikitajwa kuwa sababu kuu za kuongezeka kwa upinzani dhidi yake miongoni mwa Wamarekani.
Kulingana na tafiti mpya za YouGov, Donald Trump amepata kiwango cha juu zaidi cha tathmini hasi miongoni mwa marais 20 wa Marekani waliyochunguzwa, ambapo zaidi ya nusu ya wananchi wanauona utendaji wake wa urais kama duni au chini ya wastani.