Aliyekuwa akifanya Ibada za Usiku ndani ya Ramadhani na mwendo wake ukabadilika na tabia zake kuwa nzuri ndani ya Ramadhan, basi aendelee kuwa na tabia nzuri hivyo hivyo hata baada ya Ramadhan. Na hii ni sehemu ya wito na funzo zuri toka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).
Maulana Sheikh Hemed Jalala: "Adui Ibn Muljim (laana iwe juu yake), aliyempiga Imam Ali (a.s) kwa upanga wenye sumu kali, alijua kuwa hawezi kupambana na Imam Ali (a.s) akiwa nje ya Msikiti, hivyo akaona mbinu aliyokuwa nayo ni kumuwinda akiwa katika ibada (swala), kwani awapo katika swala huwa mwili wake na hisia zake zinatoweka Duniani, na anazungumza na Mola wake Mtukufu kama vile hayupo Duniani".