Iran imetangaza rasmi kwa mara ya kwanza kufikiwa kwa rasimu ya mwisho ya makubaliano na Marekani, huku Ijumaa ikitajwa kuwa siku ya kutiwa saini; wakati huo huo, wachambuzi wanaeleza kuwa usitishaji wa mapigano nchini Lebanon, endapo Israel itautekeleza, ni matokeo ya msimamo wa Iran wa kujumuisha suala la Lebanon katika makubaliano hayo na ustahimilivu wa Muqawama katika medani ya mapambano.
Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema kuwa Iran haitategemea ahadi za maadui katika medani ya diplomasia, akisisitiza kuwa mafanikio hupimwa kwa matokeo halisi na kwamba umoja wa wananchi umechangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha nafasi ya taifa hilo katika kukabiliana na mashinikizo ya nje.