Wachambuzi wa kijeshi wanasema lugha iliyotumiwa leo si vitisho vya kawaida, bali ni tamko rasmi kwamba Iran sasa inamiliki silaha “inayovunja mizani ya nguvu”, ambayo inaweza kufichuliwa moja kwa moja katika uwanja wa vita endapo Israel itathubutu kuchukua hatua.
Ngoma za vita zinapigwa… na simba wa Iran ameonyesha meno yake!
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Meja Jenerali Mohammad Pakpour, katika mazungumzo na Qasim al-A’araji, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Iraq, amesema kuwa: “Katika vita vya siku 12, tulishambulia kwa nguvu na usahihi mkubwa na tuliharibu malengo yote yaliyolengwa.”