Waziri wa Viwanda, Migodi na Biashara wa Iran, Mohammad Atabak, amewasili Islamabad kushiriki kikao cha 10 cha Kamati ya Pamoja ya Biashara kati ya Iran na Pakistan, ambapo viongozi wa pande zote mbili wanatarajiwa kujadili kuimarisha biashara, uwekezaji na Mkataba wa Biashara Huria (FTA).
Kikao cha kumi cha Kamati ya Pamoja ya Biashara kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Pakistan kimeanza rasmi mjini Islamabad kwa ushiriki wa mawaziri wa biashara wa nchi hizo mbili, kikilenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuongeza biashara ya pande mbili.