Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesifu uimara wa vikosi vya jeshi na mshikamano wa wananchi wa Iran, akisisitiza kuwa juhudi hizo zimeimarisha hadhi ya nchi, sambamba na kukumbuka mashahidi waliopoteza maisha katika mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran.
Mikusanyiko ya Maulamaa wa Kiislamu nchini Lebanon imesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonyesha kuwa ni rafiki mwaminifu wa Lebanon baada ya kutekeleza vitisho vyake vya kujibu mashambulizi dhidi ya vitongoji vya kusini mwa Beirut. Kundi hilo pia limetoa wito wa kuimarishwa kwa uhusiano kati ya Beirut na Tehran.
Kwa mujibu wa wachambuzi, ushiriki wa mamilioni ya wananchi wa Iran katika maandamano na mikusanyiko ya kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ni ishara ya mshikamano wa ndani na jibu la kisiasa kwa vitisho vinavyozidi kuongezeka kutoka Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.