Miungano

  • Kikao cha Siri cha Netanyahu Abu Dhabi; Hofu ya Bab al-Mandab Kurudi Chini ya Udhibiti wa Yemen

    Kikao cha Siri cha Netanyahu Abu Dhabi; Hofu ya Bab al-Mandab Kurudi Chini ya Udhibiti wa Yemen

    Kufuatia Yemen kurejesha kikamilifu mamlaka yake juu ya Mlango wa Bahari wa Bab al-Mandab na maeneo ya pwani ya magharibi, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Israel, alifanya ziara ya siri na ya dharura mjini Abu Dhabi, ambapo alishiriki katika kikao cha siri kilichowahusisha wawakilishi wa nchi kadhaa za Kiarabu, zikiwemo Saudi Arabia, Jordan na Morocco, pamoja na wawakilishi wa vikosi vinavyomuunga mkono Khalifa Haftar nchini Libya. Lengo la kikao hicho limetajwa kuwa ni kuunda muungano wa kijeshi wa kujihami utakaokuwa mbadala, kwa ajili ya kufidia kushindwa kwa vikosi hivyo katika uwanja wa vita na kusambaratika kwa muungano unaoongozwa na Saudi Arabia.