Hezbollah imesema imefanya operesheni 22 za kijeshi kwa kutumia makombora, ndege zisizo na rubani na mizinga dhidi ya vikosi vya Israel kusini mwa Lebanon, ikidai kuharibu magari ya kijeshi, kulenga vituo vya kijeshi na kulazimisha ndege ya Israel ya aina ya Hermes 450 kuondoka katika anga la Lebanon.
Rada ya Iran aina ya "Kavosh" pamoja na mizinga ya HM-40 vimeonekana katika gwaride la kijeshi nchini Armenia, jambo linaloashiria kuendelea kwa ushirikiano wa kijeshi kati ya Tehran na Yerevan.