Mohammad Mokhber, Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, amesema kuwa vitisho vya Donald Trump vinatokana na kipigo alichopokea kutoka kwa Iran, akisisitiza kuwa wapiganaji wa Iran, kwa kutegemea uungaji mkono wa wananchi, watampiga Trump pigo la mwisho na kumweka katika mipaka yake.
Mshauri wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Mohammad Mokhber, amesema Iran haitakubali makubaliano yasiyotekelezwa kikamilifu na kusisitiza kuwa haki za wananchi wa Iran pamoja na damu za mashahidi haziwezi kusahaulika.